Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi kusuka upya kikosi Yanga

MWAMBUSI Mwambusi kusuka upya kikosi Yanga

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya kulazimishwa sare ya bao 1-1, jana Jumamosi na KMC nyumbani kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kocha mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi ameeleza kurudi kambini kusuka kikosi kwaajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu na Kombe la Azam.

Katika mechi hiyo ambayo ni ya kwanza ya kimashindani kwa Mwambusi kuiongoza yanga akiwa kaimu kocha mkuu hapo, Mwambusi alinukuliwa akisema kuwa baadhi ya wachezaji wake hawakuwa kwenye kiwango bora kama alivyotarajia.

"Hayakuwa mategemeo yetu kupata matokeo yale lakini ndivyo mpira wa miguu ulivyo, baadhi ya wachezaji hawakuwa katika kiwango tulichotegemea jambo lililotukosesha alama tatu muhimu," alisema Mwambusi na kuongeza:

"Nimeona matatizo hayo, tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia marejeo na masahihisho na kuhakikisha kila nafasi tutakayoitengeneza inatumiwa vizuri na kutupa matokeo chanya," alisema.

Licha ya kupata sare katika mchezo huo, Yanga bado ni vinara kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na alama 51 baada ya kucheza mechi 24 na kushinda 14, sare tisa na kupoteza mechi moja pekee.

Mchezo unaofuata Yanga watakuwa nyumbani kuwakabiri Biashara United ya Mara ambayo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa April 17 kwenye dimba la Mkapa.

Related Kumbe KMC waliipania Yanga!



Simba SC, Yanga zapewa mchongo Mastaa Yanga wachimba mkwara!
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz