Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi aahidi taji Yanga

24db0675d5451daf949fddf514702535 Mwambusi aahidi taji Yanga

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema atahakikisha mabingwa hao wa kihistoria wanarudi katika ubora wao uliopotea kwa muda mrefu na kutwaa mataji.

Mwambusi aliyewahi kuifundisha timu hiyo akiwa na Kocha Hans Pluijm aliisaidia Yanga kutwaa mataji matatu na kati ya hayo, mawili ya ligi na moja la FA kabla ya kutimuliwa na sasa kurejea tena.

Akizungumza na gazeti hili, Mwambusi alisema anajua namna kutakavyokuwa na ushindani ila wanajipanga akiamini uwezo wanao kama tu wataendelea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi.

“Nawashukuru Yanga kwa kunirejesha, tutajitahidi kurejesha furaha iliyokuwa imepotea, tunaendelea na maandalizi naamini mambo yatakuwa mazuri, kwani lengo letu ni kuchukua taji msimu ujao,”alisema.

Kocha huyo atasaidiana na Kocha Mkuu Mserbia Zlatko Krmotic aliyetangazwa na klabu hiyo juzi baada ya aliyekuwa akitarajiwa kujiunga nao Mrundi Cedrick Kaze kushindwa kuwa nao kutokana na matatizo ya kifamilia.

Mserbia huyo anatarajwa kuwasili nchini leo kutoka kwao Yugoslavia kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuwa kocha mpya wa klabu ya Yanga.

Krmpotic mwenye umri wa miaka 62, mzaliwa wa Belgrade, ni kocha mwenye uzoefu mkubwa aliyeanzia kwenye kucheza soka katika nafasi ya ulinzi.

Kati ya mwaka 1977 na 1986, Krmpotic aliichezea mechi zaidi ya 200 za mashindano yote klabu ya Red Star Belgrade ya kwao kwa misimu tisa, na kushinda mataji matano.

Aliwahi pia, kucheza Uturuki katika klabu ya Genclerbirligi kati ya 1986 na 1988 kabla ya kurejea nyumbani kwao kumalizia soka yake katika klabu ya AIK Backa Topola.

Krmpotic pia aliichezea timu ya taifa ya ya Yugoslavia mechi mbili katika fainali za Kombe la Duna mwaka 1982, timu hiyo ikimaliza kwenye nafasi ya tatu hatua ya makundi.

Aliwahi kushinda Kombe la Matafa ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 ‘UEFA Euro U-21’ mwaka 1978 akiwa na Yugoslavia.

Na tangu awe kocha, Krmpoti?amefundisha klabu tofauti katika nchi 12 duniani, ambazo ni AIK Ba?ka Topola, OFK Beograd za Serbia, Degerfors IF ya Sweden, Sloga Jugomagnat ya FYR Macedonia, Ankaragücüya Uturuki, Paniliakos ya Ugiriki, Nea Salamis ya Cyprus, Kairat ya Kazakhstan na Kazma ya Kuwait.

Nyingine ni Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ZESCO United ya Zambia, Jwaneng Galaxy ya Botswana, APR ya Rwanda, Polokwane City na Royal Eagles za Afrika Kusini.

Pia, alizifundisha timu za taifa za vijana za Serbia na Montenegro chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2005 na U19 ya Serbia 2007 na 2008.

Aliwahi kushinda tuzo za Kocha Bora wa DRC msimu wa 2016-2017, Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Zambia msimu wa 2017-2018, Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Botswana mwaka 2018 na Kocha Bora wa Afrika 2017-2018.

Chanzo: habarileo.co.tz