Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalala ashangaa kuhusishwa kutua Yanga

83044 Pic+mwalala Mwalala ashangaa kuhusishwa kutua Yanga

Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Tetesi inasambaa kwa kasi sana. Inasambaa kama Upepo. Hata kabla haijathibitika kwamba, miamba wa soka nchini Tanzania, Yanga SC wameivunjilia mbali benchi la ufundi, tayari jina lake lilianza katajwa. Siyo katika majukwaa ya Soka kwenye mitandao ya Tanzania, hadi huku Nairobi na Mombasa, jina la nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa Bandari FC ya Kenya, lilikuwa linatrendi. Mwinyi Zahera, ambaye ni raia wa Congo, pamoja na benchi lake lote la ufundi, isipokuwa kocha wa makipa, Peter Manyika, ameoneshwa mlango wa kutokea ikiwa ni mbili baada ya kubanduliwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na klabu ya Pyramids ya Congo. Hata hivyo, taarifa zilizoifikia Mwanaspoti ni kwamba, Bernard Mwalala ambaye anajulikana kwa hulka yake ya kuongea maneno machache, alipoliona jina lake likitrendi alishangaa sana. Mwalala ni mmoja wa nyota wachache kutoka Kenya, pamoja na Boniface Ambani, wenye heshima na historia kubwa ndani ya klabu hiyo yenye makao yake mitaa ya jangwani, alisisitiza kuwa hakuna mawasiliano ya aina yoyote na Yanga. "Unajua hata mimi nimeshangazwa Sana na taarifa hizi, kifupi nikuambie tu kuwa, ndio kwanza nasikia habari hizo. Sijaongea nao. Bado nina mkataba na Bandari, Concentration yangu iko Bandari," alisema Mwalala Wakati hayo yakiendelea, tayari Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla amememtangaza Charles Boniface Mkwasa, kushika wadhifa huo kwa muda hadi pale kocha mpya atakapotangazwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz