Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakyembe apewa somo Simba

69958 Pic+mwakyembe

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MGENI rasmi wa shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika uwanja wa Simba uliopo Bunju B, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe mara baada ya kiwasili alipewa somo.

Mwakyembe baada ya kufika hapa saa 5:02 asubuhi alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Mohammed Dewji 'Mo Dewji'.

Baada ya kufika Mwakyembe alipelekwa katika uwanja ambao unaandaliwa kuwekwa nyasi bandia.

Mo Dewji baada ya kumpokea alimwelekeza Mwakyembe kuwa viwanja hivyo kabla ya kufika mwezi Disemba mwakani vitakuwa vimekamilika hasa eneo la kuchezea.

Mo Dewji alisema viwanja hivyo viwili vimejengwa kutokana na ujuzi walioupata kutoka timu nyingine kubwa.

"Tunaendelea kujenga uwanja wa nyasi bandia ili kuutumia kama tutakwenda kucheza mechi viwanja kama hivyo kama vile ambacho walikwenda kutumia katika mechi na TP Mazembe,"

Pia Soma

"Lakini tumeweka kiwanja chenye nyasi bandia kutokana tutacheza viwanja vyenye nyasi bandia kama kile ambacho tulicheza na JS Soura.

"Lakini miundo mbinu ambazo tumeweka viwanja hivi niliona katika nchi za Ureno nilipokwenda kutembelea timu ya FC Porto na hata nilipofika pale Ujerumani na tumeamishia hapa kwetu," alisema Mo Dewji.

Mwekyembe baada ya kupata somo hilo alionekana kutingisha kichwa na kuwapongeza viongozi wa Simba.

"Hongereni sana uongozi wote wa Simba hakika mmefanya kazi kubwa katika mradi huu mkubwa hapa nchini," alisema Mwakyembe.

Chanzo: mwananchi.co.tz