Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo kuzichapa Oktoba Dar

74380 Mwakinyo+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BONDIA Hassan Mwakinyo kwa mara ya kwanza atapanda ulingoni kuzichapa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Oktoba 26.

Mwakinyo ambaye ni balozi wa Sportpesa atazichapa kuwania ubingwa wa kimataifa  pambano la raundi 10 la uzani wa super welter.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema Mwakinyo atazichapa na mmoja wa mabondia kutoka kati ya nchi za Ufilipino, Italia, Marekani, Urusi au Argentina.

Alisema tayari wamezungumza na vyama vya ngumi vya kimataifa vya WBO na IBO ili Mwakinyo agombee mkanda wa ubingwa wa vyama hivyo.

Akizungumzia pambano lake, Mwakinyo alisema yuko fiti na hana hofu ya kuzichapa na bondia yoyote.

Miongoni mwa mabondia hao ni Stefano Castellucci wa Ufilipino na Arnel  Tinampay wa Itali.

Pia Soma

Advertisement
"Niko fiti, yoyote atakayekuja niko tayari kuzichapa naye bila kujali anatoka nchi gani au ina uwezo gani kwenye ngumi," alisema Mwakinyo.

Amesema amelazimika kucheza pambano Dar es Salaam ili kukata kiu ya mashabiki wake ambao tangu ametoka Uingereza alipomchapa Samm Eggington wametamani kumuona akicheza Dar es Salaam.

"Nilipata ofa ya kucheza Kenya, lakini nimekataa, nahitaji kucheza nyumbani ambako mashabiki wa ngumi kwa muda mrefu wametamani kuniona nacheza Dar es Salaam," amesema.

Akizungumzia kucheza na mabondia maarufu nchini, Mwakinyo amesema ni suala la muda tu, kwani yuko tayari kucheza na yoyote.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz