Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo amchapa Sinkala kwa TKO

24546 Pic+mwakinyo TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo ameendelea kutamba kwenye mapambano ya nyumbani baada ya jana usiku kumchapa Joseph Sinkala kwa Technical Knock Out {TKO) raundi ya pili.

Katika pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa  Mkwakwani mjini Tanga, mpinzani wa Mwakinyo alianza kupotezwa dakika ya pili ya raundi ya kwanza kabla ya kusalimu amri na kukubali kipigo cha TKO raundi ya pili ya pambano lililokuwa la raundi 10 la uzani wa super welter.

Kwa ushindi huo, Mwakinyo ametwaa mataji mawili ya kimataifa ya UBO na WBL.

"Maandalizi niliyoyafanya ndiyo yamenipa ushindi, Sinkala alianza vizuri pambano lakini hakuwa nab mbinu za ushindi, siyo bondia dhaifu, ana ngumi nzito, lakini amecheza na mbabe zaidi yake," alijinasibu Mwakinyo muda mfupi baada ya pambano hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz