Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo afuata nyayo za Tyson

24711 Pic+mwakinyo TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kumchakaza Joseph Sinkala kwa Technical Knock Out (TKO) na kutwaa mataji ya kimataifa ya WBL na UBO, juzi usiku, Hassani Mwakinyo ametoa onyo kwa mabondia wengine watakaoingia kwenye anga zake.

Mwakinyo alimchapa Sankala raundi ya pili ya pambano ambalo mwamuzi Anthony Rutha alilazimika kulimaliza ili kumnusuru Sinkala kwa kipigo kufuatia kuchapwa makonde mfululizo yaliyompeleka chini mara mbili huku akionekana kupoteza uelekeo.

Katika pambano hilo la uzani wa super welter lililokuwa la raundi 10 lililofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Mwakinyo alionekana kuimarika tangu kengere ya kuashiria kuanza raundi ya kwanza kwa kuanzisha mashambulizi mara tu baada ya pambano kuanza.

"Halikuwa pambano jepesi pamoja na kuwa nimeshinda kwa TKO, mpinzani wangu ni bondia mzuri na kuna wakati hata mimi nilimhofia, lakini utulivu, maandalizi na kujiamini ndivyo vimenipa ushindi," alisema Mwakinyo.

Sinkala alianza kupata ugumu dakika ya pili ya raundi ya kwanza baada ya kushambuliwa makonde mfululizo bila majibu lakini akaokolewa na kengere ya kuashiria kumalizika raundi hiyo.

Raundi ya pili, Mwakinyo aliendeleza ubabe baada ya kumtandika konde zito la kulia lililompleka Sinkala chini lakini akanyanyuka na kujifuta glovu kisha kuendelea na pambano kabla ya kutandikwa tena konde lililomlevya na kumpeleka chini na refarii kuamua kumaliza pambano ili kumnusuru Sinkala kwa kipigo zaidi.

Bondia huyo alitoa angalizo kwa mabondia wa uzani wake nchini akisisitiza kuwa mkakati wake ni kumaliza pambano mapema kama alivyokuwa akifanya nguli wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Mike Tyson.

Ushindi huo ni watatu mfululizo kwa Mwakinyo kushinda kwa Knock Out (KO) na TKO tangu alipomchapa aliyekuwa bondia namba nane wa dunia kwenye uzani wa super welter, Sam Eggington nchini Uingereza, pambano lililompa umaarufu na kuacha mshtuko kwa wadau wa ndondi nchini humo kutokana na rekodi ya Eggington.

Baada ya pambano hilo la Uingereza, Mwakinyo alicheza mjini Tanga na Said Yazidu na kumchapa kwa KO sekunde ya 47 Kabla ya Juzi Usiku kumchakaza kwa TKO, Sinkala.

Chanzo: mwananchi.co.tz