Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Mfilipino Tinampay nitamchakaza mapema

85711 Pic+mwakita Mwakinyo: Mfilipino Tinampay nitamchakaza mapema

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Bondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay wametambia kila mmoja akijinasibu kushinda katika pambano lao la Novemba 29 litakalofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabondia hao leo Jumapili wakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza kwenye viwanja vya Leaders, Dar es Salaam mbele ya mashabiki zao.

Tinampay ndiye alikuwa wa kwanza kuwasili uwanjani hapo akiwa amepanda moja ya pikipiki kati ya 10 zilizomsindikiza nyingine wakiwa wamepanda mashabiki wake raia wa Ufilipino.

Dakika chache baadae, Mwakinyo aliwasili na kushangiliwa kwa nguvu na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuwashuhudia kabla ya Mwakinyo kuanza kumtambia Tinampay akimwambia ameingia sehemu tofauti.

"Huyu Mfilipino si saizi yangu, nitampiga kipigo ambacho atakwenda kusimulia nchini kwao, ameingia anga nyingine," alijinasibu Mwakinyo.

Alisema amejiandaa kwa matokeo ya Knock Out ya mapema, hivyo mashabiki wake wakichelewa uwanjani, watapishana na pambano.

Huku akishangiliwa kwa nguvu, Mwakinyo alisema Tinampay ni kama chipukizi kwake, licha ya kuwa ana uzoefu wa kutosha kulinganisha na yeye.

Tinampay alijibu mapigo akidai hawezi kupigwa na Mwakinyo, ingawa amesisitiza kuwa anatarajia baada ya pambano hilo watakuwa marafiki.

"Nimewapenda Watanzania kwa ukarimu wao, lakini kwa Mwakinyo watanisamehe, nimetoka Ufilipino kuja kufanya kazi, asitarajie mteremko," alisema Tinampay.

Chanzo: mwananchi.co.tz