Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakalebela afungiwa kujihusisha na soka

MWAKALEBELA 1 Mwakalebela afungiwa kujihusisha na soka

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amefungiwa kujihusisha na soka na Kama ya maadili ya shirikisho la soka nchini TFF kwa muda wa miaka mitano baada ya kukutwa na makosa ya uchochezi na kusema uongo juu ya mkabata wa mchezaji Bernard Morrison na klabu ya Simba.

Mwakalebela amekutwa na makosa hayo baada ya kushindwa kutoa ushahidi wa juu ya tuhuma zake na bodi ya ligi, chama cha waamuzi na TFF kuwahujumu Yanga pamoja na suala la koenesha mkataba wa Morrison ambao si wa kweli.

(Taarifa ya kumfungia Mwakalebela iliyotolewa asubuhi ya leo tarehe 2 Aprili na kamati ya maadili ya TFF.)

Chanzo: eatv.tv