Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yatia doa uhakiki wa kadi Yanga

55755 MVUA+PIC

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimevuruga ratiba ya uchaguzi wa Yanga unafanyika leo katika bwalo la Polisi.

Uchaguzi huo umeanza kwa wanachama kujiandikisha, kadi zao kukaguliwa na baadaye kuhakikiwa saa mbili kama ratiba ilivyojieleza na kumalizika saa nne, lakini kutokana na mvua idadi ya wanachama wanaojitokea imepungua.

Mwanaspoti limefika eneo la tulio na kushuhudia wanachama namna wanavyoingia na kuhakikiwa kitu ambacho hakiwezi kukamilika kwa muda uliopangwa.

Akizungumzia tatizo hilo, Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela alisema kuhakikiwa kwa kadi ni muhimu na kuweka wazi kuwa ni kadi zote zitatumika.

Alisema hawawezi kupingana na mahakama kuhusiana na kupitishwa kwa matumizi ya kadi zote kutumika na kuongeza kuwa kikubwa kinachofuatiliwa ni uhakiki tu ili mwanachama aweze kupata nafasi ya kupiga kura.

Utulivu watawala uchaguzi Yanga

Hali ni ya Utulivu kwenye uchaguzi wa Yanga huku wanachama wakidai manyanyaso Mwisho leo.

Licha ya changamoto ya mvua katika Maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam wanachama wamejitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo.

Wanachama hao wameonyesha Utulivu tangu kujiandikisha, kuhakikiwa hadi kuingia ukumbini ambapo walihamasishana kutofanya makosa.



Chanzo: mwananchi.co.tz