Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukoko: Nimekuwa Nikipitia Wakati Mgumu

Mukoko Yanga Mukoko Tonombe

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIUNGO wa Yanga, Mukoko Tonombe amefunguka sababu ya kumwaga machozi baada ya kufunga bao katika mechi yao ya juzi, Alhamisi, Novemba 2, 2021 katika Dimba la Mkapa dhidi ya Ruvu Shooting.

“Nimekuwa nikipitia wakati mgumu, msimu uliopita baada ya kupata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Simba mambo yamekuwa sio mazuri kwa maisha yangu ya soka,” amesema Mukoko na kuongeza.

“Kuna wakati nilijikuta nakata tamaa na kulia nikiwa peke yangu kambini na nyumbani ndio maana baada ya kufunga nilijikuta nalia kwa furaha iliyochanganyikana na uchungu.

"Niwashukuru mashabiki wote wa Yanga walioonyesha kuwa nami katika kipindi chote kigumu. Nawaahidi kuwapa raha zaidi.” - Mukoko Tonombe Kiungo Yanga Sc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live