Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muivory Coast wa Simba kumbe mtaalamu wa 'derby'

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zana ambaye alitua jijini Dar es Salaam juzi Jumatano akitokea kwao Ivory Coast na moja kwa moja akaenda kuishuhudia Simba ilipokuwa ikiivaa Mbabane Swallows ya Eswatini.

Amesema, hana wasiwasi na mchezo wa 'derby' kama pale Simba itakapokutana na Yanga kwa sababu anajua kinachotumika hapo ni akili tu.

"Mchezo wa 'Derby' kwa kawaida kinachomaliza ni mpango mzima wa saikolojia na uwezo wa kichwa chako katika kwenda sawa na matukio utakayokutana nayo,"alisema Zana jina ambalo hata mwenyewe anapenda aitwe hivyo.

Amesema, anajua kunapochezwa mechi ya namna hiyo, kuna ushindani mkubwa kutoka timu zote, mashabiki na mambo mengine mengi: "Unapotuliza akili na kuzuia changamoto zote kila kitu kinakwenda sawa."

Simba na Yanga watakutana kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara pia upo uwezekano wa kukutana katika mashindano mengine kama Kombe la Mapinduzi na Sportpesa.



Chanzo: mwananchi.co.tz