Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muivory Coast wa Simba kibaruani leo

32439 Pic+simbaaa Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Beki mpya wa Simba, Coulibaly Zana leo Jumatano jioni atacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya KMC tangu asajiliwe na mabingwa hao Ligi Kuu Bara.

Zana raia wa Ivory Coast amesajiliwa Simba kuzipa pengo la Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi na atakaa nje kwa zaidi ya miezi miwili tangu aanze matibabu mwezi uliopita.

Zana ameiambia Mwanaspoti Online kwamba ni furaha kubwa kwake kuhakikishiwa kucheza mechi hiyo tangu ajiunge Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

"Nina furaha kubwa sana leo, kocha ameniambia nitacheza mechi yangu ya kwanza, kikubwa namuomba Mungu nifanye vizuri, nimejiandaa na nimefanya mazoezi kulingana na programu ya mwalimu aliyonipa," alisema Zana.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alimpa programu maalumu beki hiyo wakati wenzake wanaipigania klabu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo sasa inajiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Nkana Red Devils itakayochezwa wikiendi hii.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz