Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Mtwara kuchele’ mapokezi ya Yanga SC yafana kabla ya kuikabili Ndanda FC (video+picha)

3939 Yanga 1.png

Mon, 5 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Bingwa mtetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imepata mapokezi ya kutosha wakati wakiwasili Mtwara kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Ndanda FC utakao pigwa katika dimba la Nangwanda  hapo kesho siku ya Jumatano.

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya mwisho hii leo kabla ya kuelekea katika mchezo huo muhimu huku kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina akisema kuwa timu yake ipo tayari kuivaa Ndanda FC.

Kupitia kwa msemaji wa Yanga SC, Dismasi Ten amesema kuwa ameshakiandaa kikosi chake vizuri kwaajili ya kupata matokeo katika mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuweza kusonga mbele.

Chanzo: bongo5.com