Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa yakanusha kuachana na kocha Hitimana

Hitimana.jpeg Mtibwa yakanusha kuachana na kocha Hitimana

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Turian Morogoro Nassor Aboubakar amethibitisha kutokuachana na kocha Hitimana Thierry raia wa Burundi.

Submitted by Tigana Lukinja on Alhamisi , 15th Apr , 2021 Kocha Hitimana Thierry

Akizungumza na Kipenga ya East Africa Radio Nassoro alisema'' Mwalimu alituaga anakwenda likizo nyumbani Burundi ili kutatua matatizo ya kifamilia,tulimpa likizo kama mfanyakazi mwingine anapitia changamoto za kibinadamu''.

Alipo ulizwa juu ya tetesi za kocha huyo kufanya kazi na Mtibwa bila mkataba alijibu kwa kujiamini ''Hitimana ni kocha wetu na bado tunamkataba naye, huwezi kufanya kazi na taasisi kubwa kama ilivyo Mtibwa bila kuwa na mkataba alisema Mwenyekiti huyo.

Kuhusu taarifa kwamba Hitimana ameondoka kupitia mahusiano mabovu na wasaidizi wake hali iliyomfanya kushindwa kufanya vizuri alisema '' sisi kama uongozi tunaamini hakukuwa na mpasuka wowote kwa sababu tunaishi kama familia.

Kipenga ilivyombana zaidi juu ya hatma ya kocha huyo na muda uliyobaki kama wanaweza kumuajiri kocha mwingine kwa wakati huu ili kumalizia mechi zilizobaki alisema'' tunaenda kujadili kama uongozi,kikao kitakacho tupo dira ya timu yetu na kujua kama kuna mahitaji ya moja kwa moja ya kocha mwingine''

Mtibwa Sugar haifanyi vizuri kwa sasa, ipo kwenye nafasi ya 15 miongoni mwa timu 18 ikiwa na alama 24 katika michezo 24 ambapo katika msimu huu timu 4 zinazoshuka moja kwa moja na 2 zinacheza mechi za mtoano.

Chanzo: eatv.tv