Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa yakamia kubeba ubingwa

Mon, 23 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na sasa akili yake ipo kwenye mechi ya fainali.

Mtibwa ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa CCM Kambarage na sasa inasubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali nyingine itakayochezwa kesho kati ya Singida United na JKT Tanzania.

Mabao ya Mtibwa Sugar katika mechi hiyo yalifungwa na Hassan Dilunga katika dakika ya 30 na 38.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mechi hiyo, Katwila alisema timu yake ilijipanga kushinda mechi hiyo baada ya kupoteza kwa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi.

Katwila alisema baada ya kipigo hicho aliamua kuongea na wachezaji wake na kuwajenga kisaikolojia kuwa watashinda na kusonga mbele katika mchezo wao wa fainali. Alisema katika ushindi wao dhidi ya Stand United wachezaji wake walicheza vyema na kufuata maelezo yake jambo lililowapa ushindi.

Aliahidi timu kwamba, timu yake itajipanga kupata ushindi katika mechi ya fainali itakayochezwa Juni 2 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo Mtibwa itakosa nafasi hiyo kwani inatumikia adhabu ya kukosa michuano mitatu iliyopewa na Shirikisho la Soka Afrika CAF zaidi ya miaka sita iliyopita.

Chanzo: habarileo.co.tz