Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa matumaini, Coastal yabanwa

592142a3fdacc8d8a150cbba2a9f00cb Mtibwa matumaini, Coastal yabanwa

Thu, 22 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KLABU ya soka ya Mtibwa Sugar imeonesha matumaini ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao, baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa mtoano dhidi ya Transit Camp, huku Coastal Union ikibanwa ugenini dhidi ya Pamba.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mtibwa ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Timu ya Daraja la Kwanza Transit Camp na kubakiza matumaini ya kuendelea kuwepo.

Mabao yalifungwa na Ibrahim Ahmada matatu dakika ya (9, 70, 84), Kelvin Sabato dakika ya 12 na kuifanya Mtibwa kuondoka kifua mbele kwa idadi kubwa ya mabao huku la Transit likifungwa na Karegea Hazanga dakika ya 16.

Kwa ushindi huo, Mtibwa inahitaji matokeo ya sare au ushindi wowote katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ili kuendelea kucheza msimu ujao.

Kwa upande wa Coastal Union imebanwa ugenini dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza ya Pamba kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Coastal ilitangulia kupata bao la uongozi dakika ya kwanza lililofungwa na Abdul Suleiman na dakika ya 12 James Ambrose alisawazisha. Dakika ya 77 wakapata bao la pili la penalti likifungwa na Emanuel Haule kabla ya Coastal kusawazisha dakika ya 88 kupitia kwa Raizin Hafidh.

Pamba FC walikosa mkwaju wa penalti uliopigwa na Elinywesya Simbu katika dakika ya tano baada ya nahodha wa timu hiyo, Majaliwa Shaban kuangushwa eneo la hatari.

Mchezo wa marudiano wa Coastal na Pamba utakaochezwa Jumamosi mkoani Tanga ndio utakaoamua wa kubaki au kupanda.

Coastal ikipata sare tasa, bao 1-1 au ushindi wowote atakuwa na nafasi ya kubaki msimu ujao au Pamba inahitaji ushindi kuanzia bao 1-0 na kuendelea kujihakikishia nafasi ya kupanda Ligi Kuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz