Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa kufa na Yanga

996b70524d249248bb0642615c884c28 Mtibwa kufa na Yanga

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Mtibwa Sugar imetangaza mchezo unaokuja dhidi ya Yanga hawawezi kukubali kupoteza kirahisi kwakuwa wanahitaji ushindi ili kujitengenezea mazingira ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Mtibwa ambayo kwa sasa ipo kwenye ukanda mbaya katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa katika nafasi ya 14 baada ya kufikisha pointi 41 wakicheza michezo 36, wanahitaji ushindi kwenye michezo miwili iliyosalia dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro Kocha wa timu hiyo Zuber Katwila alisema bado kikosi chake kina nafasi ya kuendelea kupamba kwenye michezo iliyosalia na watahakikisha wanabaki katika ligi msimu ujao.

“Tupo kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo,lakini hatuwezi kukata tamaa bado tuna mechi mbili,ambazo zinaweza kuamua hatma yetu ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao,“ lisema Katwaila.

Alisema mchezo huo utakuwa kama fainali kwao lakini hawatawabeza Yanga wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, kwani nao wanapigania kumaliza ligi wakishika nafasi ya pili.

Mtibwa wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na morali ya chini baada ya kutoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya KMC kwa bao 1-0, wakati wapinzani wao Yanga walitoka kuambulia sare mbele ya Mwadui FC mechi iliyofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Chanzo: habarileo.co.tz