Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar yaweka dau kumnasa nyota Yanga

Yanga 0 Kiungo Said Juma Ally Makapu, Yanga SC

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kocha Mkuu wa Klabu ya Kagera Sugar, Mohamed Badru,ameonesha kumtaka kiungo wa Yanga SC,Juma Makapu, ambaye amemtaja kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, beki wa kulia na wa kati.

Alisema katika ripoti yake amependekeza nafasi za wachezaji anaotaka wasajiliwe, huku akisisitiza kuwataka wachzaji wenye uzoefu na uwezo wa kukabiliana na ushindan iuliopo katika mechi za ligi kuu Tanzania Bara

Kocha huyo alisema hawezi kuweka wazi majina ya wachezaji wengine kwa sababu kuna wengine wanawindwa na timu nyingine, hivyo zinaweza kuongeza ushindani.

"Kuna wachezaji nimewataja majina, kwa sasa siwezi kuweka wazi majina hayo, ila tusubiri viongozi wafanyie kazi ripoti yangu kama nilivyopendekeza, ninahitaji beki wa kulia, beki wa kati na kiungo mkabaji," alisema Badru.

Aliongeza kusema kuwa msimu uliopita walimaliza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa presha, hivyo wanajipanga kujiimarisha kwa kufanya usajili makini, ili makosa yaliyojitokeza yasijirudie.

"Hatutaki kujiweka katika presha kubwa kama ilivyokuwa msimu uliopita, hatutaki kurudia makosa yale yale, tumejipanga kufanya vizuri katika michezo yote ya ligi na Kombe la FA," Badru alisema.

Aliongeza anafahamu kila timu iko kwenye mchakato wa kuimarisha kikosi chake na wao wanahitaji kukamilisha malengo yao mapema na kuanza maandalizi ya msimu mpya kama walivyopanga.

Chanzo: ippmedia.com