Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar yaikalisha Yanga uwanjani ikiifunga bao 1-0

52803 Pic+matokeo

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Timu ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Bao la Mtibwa Sugar liliwekwa wavuni na Riphat Khamis dakikaya 52 kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo Mtibwa Sugar imefikisha pointi 48 ikiwa nafasi ya tano huku Yanga wakiendelea kuwapo kileleni na alama 74.

Awali kabla ya mchezo kuanza, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alielezea kusikitishwa na bodi ya ligi TBL kubadilisha muda wa kucheza mechi yao na Mtibwa Sugar kutoka saa 10:00 jioni hadi saa 8:00 mchana kwamba inawaumiza wachezaji wao.

 

Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF), jana kupitia kwa msemaji wake  Clifford Ndimbo walitoa taarifa ya kurudisha nyuma muda wa kucheza mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Simba na Coastal Union (Mkwakwani).

Kitendo hicho kimemuumiza kocha Zahera aliyedai wachezaji ni binadamu wanapaswa kuangaliwa wanapopanga mechi zao kujua maumivu ambayo wanayapata.

"Wachezaji sio chungwa wala mbuzi ni binadamu, haiwezekani mechi kutoka saa 10:00 jioni kuirudisha nyuma mpaka saa 8:00 hali ya hewa inakuwa inawaumiza kupita kiasi.

"Kama ni michuano ya AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ambayo Tanzania ni wenyeji ratiba yao ilikuwa inajulikana tangu mwanzo, inapotokea haya inaumiza.

"Ushauri wangu upangaji wa ratiba uzingatie na afya za wachezaji pia wanaumia kwa kuwa wanatumia damu,"anasema.



Chanzo: mwananchi.co.tz