Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar wa kimataifa mambo yao taratibu!

29580 Pic+mtibwa TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtibwa Sugar inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam lakini kitu kipya ni kwamba, baada ya kuweka mipango yao sawa, wataondoka wote siku ya Jumapili kuifata Northern Dynamos ya Shelisheli.

Walichofanya Mtibwa Sugar ni tofauti na ilivyo kwa vikosi vingine kama Simba, Yanga au Azam FC wanapokuwa na michuano ya namna hiyo huwa wanatanguliza watu kwa ajili ya kuweka mambo sawa.

Meneja wa Mtibwa Sugar, David Bugoya amesema, kila kitu juu ya safari yao kimekaa sawa na ndiyo maana wanajiamini na wanachokifanya.

"Kwa taarifa za awali ilikuwa atangulie kiongozi mmoja kwenda Shelisheli lakini baada ya kutathmini mpango mzima ikaonekana vizuri tukaondoka pamoja na mipango yote iko sawa,"alisema Bugoya.

Akizungumzia mazoezi yao, Bugoya alisema timu inajifua kwenye Uwanja wa Uhuru kwa kipindi chote hadi watakaposafiri kwenda Shelisheli.

Mtibwa Sugar na Northern Dynamos watacheza mechi ya marudiano Jumanne ijayo nchini Shelisheli. Katika mechi ya awali Mtibwa Sugar iliichapa Northern Dynamos mabao 4-0, mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.



Chanzo: mwananchi.co.tz