Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar na yenyewe yatoka kwa 5-1 Shirikisho

33036 Mtibwa+pic Tanzania Web Photo

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ni kama vile mwosha huoshwa. Mtibwa Sugar imetupwa nje ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jana kuchapwa mabao 2-1 na KCCA ya Uganda katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Turiani Morogoro imetolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Uganda wiki iliyopita.

Mtibwa ilikata tiketi ya kucheza na KCCA baada ya kuitoa Diamond ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 5-0, ikishinda 4-0 Dar es Salaam na 1-0 ugenini.

Katika mchezo wa jana, tatizo la Mtibwa liliendelea lilelile la kushindwa kutengeneza nafasi za mabao na kupungua kwa umakini kwenye safu yao ya ulinzi ni kati ya mambo yaliyosababisha Mtibwa Sugar kupoteza mchezo huo.

Kupungua kwa umakini kwenye safu ya ulinzi ya Mtibwa Sugar dakika ya 28, kulisababisha waruhusu bao, baada ya kushindwa kumdhibiti Allan Okello aliyemtengenezea pasi Muzamiru Mutayaba na kufunga bao hilo. Mtibwa Sugar ilisawazisha bao hilo dakika ya 51 lililofungwa na Salum Kihimbwa kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na Salum Kanoni.

Baada ya kulisakama lango la KCCA ili kuongeza bao bila mafanikio, dakika ya 87, Mtibwa Sugar wakajikuta wanaruhusu bao la pili lililolofungwa na Allan Okello ambaye alipokea pasi kutoka kwa Lawrance Bukenya na kuzima kabisa fikra za Mtibwa kuingia hatua ya makundi.



Chanzo: mwananchi.co.tz