Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar kibaruani dhidi ya Njombe Mji VPL

1627 IMG 20180116 WA0038 640x360 TZW

Sat, 20 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Mtibwa Sugar inataraji kushuka dimbani leo jioni kuwakabili Njombe Mji katika uwanja wake wa nyumbani Manungu Complex, kuelekea mtanange huo kocha mkuu wa kikosi cha wana tam tam, Zuber Katwila amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwa kila upande hasa ukizingatia timu zote ziliibuka na alama tatu katika michezo yao ya mwasho kabla ya kukutana.



Kocha mkuu, Zuber Katwila ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na mtandao wa klabu hiyo.

“Mchezo huo ni muhimu sana kwetu na kwao pia hivyo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu imetoka kupata pointi tatu muhimu katika mechi iliyopita, hakuna timu itakayoingia uwanjani kinyonge zitaingia zikiwa zinahitaji ushindi na kujihami,” amesema Katwila

Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake kati kati ya shamba la miwa la Mtibwa ilifanya mazoezi yake ya mwisho siku ya Alhamisi jioni kwa ajili ya mchezo huo wa mzunguko wa 14 wa ligi kuu bara huku siku ya Ijumaa ya hapo jana waki itumia kwa mapumziko.

Timu ya Mtibwa Sugar inashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 24 katika michezo 13 huku wapinzani wao wa leo Njombe Mji wakikalia nafasi ya 13 katika msimamo baada ya kuwa na alama 11 katika mechi 13 walizocheza.

Wana tam tam msimu huu wameshinda michezo 6 , sare 6 na kupoteza mchezo mmoja hivyo kufanikiwa kukusanya pointi 24 zinazowafanya kukalia nafasi ya tatu katika msimamo na wakiwa na tofauti ya alama 5 nyuma ya vinara wa ligi Simba SC.

Chanzo: bongo5.com