Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar bado gonjwa

A7a4737ca2125051c3f289a4e54b7cbc.jpeg Mtibwa Sugar bado gonjwa

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MTIBWA Sugar imeendelea kuwa katika wakati mgumu wa kujinasua kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Gairo mkoani Morogoro.

Mtokeo hayo bado yanaifanya Mtibwa Sugar kuendelea kubaki mkiani mwa msimamo ikifikisha pointi saba katika michezo 10, huku Polisi Tanzania ikipanda hadi nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 16 katika mechi 10 ilizocheza kama ilivyo wenyeji wao Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji Vitalis Mayanga ndio alikuwa wa kwanza kuifungia Polisi Tanzania bao la kutangulia dakika ya 13, akiunganisha kwa kichwa krosi ya winga Daruweshi Saliboko na bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Mtibwa Sugar ambao wameshinda mchezo mmoja tu tangu kuanza kwa msimu huu, walikianza kwa kasi kipindi cha pili na kusawazisha bao hilo dakika ya 55 ambapo beki wa Polisi Tanzania, Datius Peter alijifunga katika harakati za kuokoa shambulizi la Mtibwa Sugar.

Kuingia kwa bao hilo kulionesha kuwazindua Mtibwa na kuanza kufanya mashambulizi mengi hasa baada ya kocha Awadhi Juma kuwaingiza washambuliaji Boban Zilintusa na Rifat Khamis ambao waliwasumbua walinzi wa Polisi ambao safu yao ya ulinzi jana ilikuwa chini ya Ally Mmanga.

Katika mchezo huo timu zote mbili zililazimika kutumia wachezaji wa vikosi vya pili kufuatia idadi kubwa ya wachezaji wao wa kikosi cha kwanza kukumbwa na ugonjwa wa kifua na mafua.

Chanzo: www.habarileo.co.tz