Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa, Coastal zabaki Ligi Kuu

6291457bf22d22c7c275251ef168f8a8 Mtibwa, Coastal zabaki Ligi Kuu

Mon, 26 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU za Mtibwa Sugar na Coastal Union ya Tanga zimefanikiwa kubaki Ligi Kuu msimu ujao baada ya kushinda mechi zao za mtoano (Play Off), dhidi ya timu za Daraja la Kwanza.

Timu hizo zimepata nafasi ya kucheza hatua hiyo ya mchujo baada ya kushika nafasi ya 13 na 14 katika msimamo wa Ligi Kuu iliyomalizika hivi karibuni.

Ushindi wa mabao 4-1 iliyoupata Mtibwa Sugar ugenini kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam uliisaidia kubaki kwenye ligi licha ya kipigo cha bao 1-0 walichopokea kwenye mchezo wa marudiano ambao umepigwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro na kufanya isongembele kwa jumla ya mabao 4-2.

Matokeo kama hayo yalikuwa kwa Wagosi wa Kaya Coastal Union, ambayo ilipata sare ya mabao 2-2 ugenini kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza kabla ya kupata ushindi wa mabao 3-1 Uwanja wa Mkwakwani jana na kuifanya timu hiyo kusalia Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3.

Beki wa Coastal Union, Peter Mwangosi aliwatanguliza mbele wageni Pamba kufuatia bao la kujifunga la dakika ya 10.

Lakini mshambuliaji chipukizi Abdallah Suleiman akaisawazishia Coastal kwa mkwaju wa penalti dakika ya 31 baada ya nahodha wa Pamba Majaliwa Shabani kumchezea rafu Raizin Hafidhi.

Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Mtibwa Sugar ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Maafande wa Transt Camp, ushindi ambao haukuweza kuivusha timu hiyo kucheza Ligi Kuu msimu ujao

Chanzo: www.habarileo.co.tz