Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania anayemsaidia staa wa Arsenal ili apate mali zake

1116 Sequence 01.Still0171 TZW

Fri, 5 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Ikiwa zimepita siku kadhaa toka staa wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast aliyekuwa anavichezea vilabu vya Arsenal ya England na Galatasaray ya Uturuki Emmanuel Eboue ajitokeze hadharani na kukiri kuwa amepoteza utajiri wake kutokana na mkewe kuchukua kila kitu baada ya kupeana talaka.

Mtanzania na mdau wa michezo anayeishi na kufanya shughuli zake nchini England Yasmin Razak ametangaza kuanza harakati za kumsaidia Emmanuel Eboue ilipatae mali zake, Eboue ambaye hivi karibuni alitangaza kuwa hana pakuishi ni rafiki wa karibu na Yasmin ambaye amejitolea kumsaidia ili apate mali zake.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri December 25 2017 Moja kati ya habari kubwa zilizochukua headlines katika upande wa michezo ni kuhusiana na stori ya Emmanuel Eboue kutangaza kupoteza utajiri wake.

Eboue kwa sasa ana umri wa miaka 34 na anaitumikia adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na FIFA kwa kushindwa kumlipa wakala wake, Eboue licha ya kutokea katika maisha magumu Ivory Coast alifanikiwa kutengeneza pesa nyingi akiwa katika Ligi Kuu England akiitumikia Arsenal kwa miaka saba.

Beki huyo wa zamani wa Arsenal aliripotiwa kuwa yupo katika maisha magumu na analala chini kwa rafiki yake huku akishindwa kulipia pesa nguo zake ziende dry cleaner, hivyo analazimika kufua kwa mikono, kikubwa kilichomfanya apoteze utajiri wake ni kumuandikisha mkewe kila kitu.

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

 

Chanzo: millardayo.com