Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva sasa apania Kiatu Ligi ya Mabingwa Afrika

Msuva Msuva sasa apania Kiatu Ligi ya Mabingwa Afrika

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza baada ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Libya mwishoni mwa wiki, ambayo Tanzania ilishinda bao 1-0 lililofungwa na yeye mwenyewe, ikiwa ni mechi ya kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), Msuva alisema lengo lake kubwa msimu huu ni kuibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa na tayari ameshapachika mabao mawili.

"Mimi kwa sasa nina magoli mawili, anayeongoza ana mabao matatu, kwa hiyo utaona bado nina nafasi nzuri tu ya kuwa mfungaji bora na hilo ndilo lengo langu," alisema Msuva.

Mbali na ufungaji bora, Msuva alisema anataka kuipa timu yake ya Wydad ubingwa wa Afrika ambapo ndiyo malengo yao msimu huu.

"Wydad ni timu kubwa sana Morocco, kama vile unavyoiona Al Ahly ya Misri, Zamalek, au hapa Tanzania Simba na Yanga. Ni timu ambayo lengo lake namba moja ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini Morocco, halafu kuchukua ubingwa wa Afrika," alisema mchezaji huyo wa zamani wa Moro United na Yanga.

Timu hiyo anayoichezea Msuva, tayari imeshafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa inaongoza kwenye Kundi C kwa pointi 10, huku Horoya ya Guinea na Kaizer Chiefs zikifuatia zote zikiwa na pointi tano mpaka sasa, kila timu ikicheza mechi nne.

Mchezaji anayeongoza kwa ufungaji mabao mpaka sasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni Ayoub El Kaabi ya Wydad ya Morocco akiwa na mabao matatu, huku Msuva wa timu hiyo hiyo, Luis Miquissone na Chris Mugalu wote wa Simba wakiwa na mabao mawili kila mmoja.

Chanzo: ippmedia.com