Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva atupia Taifa Stars yalazimisha sare kwa Burundi

74287 Msuvapic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bujumbura. Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kulazimisha sare 1-1 ugenini dhidi ya Burundi shukrani kwa bao la mshambuliaji Saimon Msuva kwenye Uwanja wa Intwari jijini Bujumbura.

Msuva alifunga bao hilo la kusawazisha akitumia vizuri uzembe wa kukosa maelewano kwa kipa wa Burundi, Jonathan Nahimana na beki wake katika dakika 84.

Wenyeji Burundi walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika baada ya makosa ya mebeki wa Tanzania kushindwa kuzia krosi iliyomkuta Amissi Cedric aliyemtoka Gadiel Michael na kupiga shuti lililomshinda kipa Juma Kaseja na kujaa wavuni.

Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kusonga mbele iwapo watapata suluhu katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar es Salaam Septemba 8, katika kuwania kutinga hatua ya makundi ya mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.

Katika mchezo huo Msuva alishindwa kutumia vyema nafasi ya kufunga bao dakika ya 17, Timu ya Taifa Stars imetawala mechi yake dhidi ya Burundi.

Msuva alipoteza nafasi hiyo muhimu baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa Jonathan Nahimana wa Burundi.

Pia Soma

Advertisement
Nyota huyo wa Difaa el Jadida alipokea pasi nzuri kutoka kwa Salum Abubakar na akiwa anamtazama Nahimana, alipiga shuti lililopanguliwa na kipa huyo na kushindwa kuipatia Stars bao la kuongoza.

Ni mechi ambayo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza imetawaliwa na Stars ambayo imekuwa ikimiliki mpira kwa kupiga pasi na kutengeneza nafasi kulinganisha na wenyeji ambazo hata hivyo hazijatumiwa vizuri.

Mfano wa nafasi hizo ukijumuisha na ile ya Msuva ni ile ya dakika ya 14 ambapo beki Diamanti Ramazani nusura ajifunge wakati alipokuwa anataka kuokoa krosi ya Mbwana Samatta lakini kipa Nahimana aliwahi kuokoa hatari hiyo.

Lakini katika dakika 15 za mwisho za kipindi cha kwanza, Burundi walibadilika na kutawala mchezo huo huku wakitengeneza nafasi kadhaa ambazo hata hivyo hawakuweza kuzitumia

Miongoni mwa nafasi hizo ni ile iliyopotezwa na Caleb Binyeminyana mnamo dakika ya 38 ambapo alimtoka vizuri Haruna Shamte na kupiga shuti lililopita pembeni kidogo ya lango.

Katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza Duhayindavi Gael nusura aipatie Burundi bao la kwanza lakini shuti lake lilitoka nje.

Katika kipindi hicho cha kwanza, wachezaji Salum Abubakar 'Sure Boy' na Duhayindavi Gael kwa upande wa Burundi walionyeshwa kadi za njano kwa kucheza rafu.

Burundi ililazimika kufanya mabadiliko ya mapema mnamo dakika ya 17 kwa kumtoa Pierre Kwizera aliyeumia na kumuingiza Duhayindavi Gael.

Dakika ya 41, Burundi walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Bimenyimana Caleb na kumuingiza Cedric Amissi

Taharuki ilizuka uwanjani hapo wakati wa mapumziko baada ya kutokea rabsha baina ya askari na  mtunza vifaa wa Taifa Stars, John Mashaka.

Askari hao walikuwa wanamzuia mashaka kuingia vyumbani mara baada ya filimbi ya kuashiria mapumziko kupulizwa wakidhani sio sehemu ya maofisa wa benchi la ufundi

Burundi hatari kipindi cha pili

Safu ya ulinzi ya Taifa Stars ipo kwenye wakati mgumu mbele ya washambuliaji wa Burundi tangu kipindi cha pili cha mechi baina yao leo kilipoanza.

Burundi ambayo ilielemewa kwenye kipindi cha kwanza, imezianza dakika 45 za pili kwa kasi kubwa na kufanya mashambulizi ya mfululizo langoni mwa Stars.

Mabadiliko ambayo Burundi waliyafanya mwishoni mwa kipindi cha kwanza kwa kumtoa Bimenyimana Caleb na kumuingiza Abdoul Fiston yameonekana kuwaimarisha na kutawala mchezo huo.

Dakika sita tu mara baada ya kipindi cha pili kuanza, Fiston nusura aipatie bao Burundi baada ya kupenya na kuingia kwenye eneo la hatari lakini kipa Juma Kaseja aliwahi kuondosha hatari hiyo.

Dakika ya 55 Stars walimtoa Hassan Dilunga na kumuingiza Iddi Seleman 'Nado' na dakika 10 baadaye walimtoa Abubakar Salum 'Sure Boy' na kumuingiza Frank Domayo.

Pamoja na mabadiliko hayo, Burundi waliendelea kutawala mchezo na kulishambulia lango la Stars kama nyuki.

Mabadiliko ambayo Burundi waliyafanya kwa kumtoa Kanakimana Bienvenu na kumuingiza Mohamed Amissi  yalizaa matunda baada ya timu hiyo kupata bao la kuongoza dakika ya

Amissi alifanya kazi ya ziada upande wa kushoto kwa kuwatoka Shamte na Himid Mao lisha kumimina majaro yaliyounganishwa vyema na Cedric Amissi.

Hata hivyo bao hilo la Burundi lilidumu kwa muda mfupi tu kwani Msuva mnamo dakika ya 84 aliisawazishia kwa kuunganisha vyema mpira uliookolewa vibaya na kipa Jonathan Nahimana uliopigwa kutokea kwenye safu ya ulinzi ya Stars.

Chanzo: mwananchi.co.tz