Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva afurukuta Difaa ikilazwa 2-1

11681 Msuva+pic TanzaniaWeb

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Algiers, Algeria. Mshambuliaji mahiri wa Tanzania, Simon Msuva, jana alitokea benchi na kuifungia Difaa El Jadidi bao la kufutia machozi ikifungwa mabao 2-1 na ES Setif ya Algeria, katika mechi ya mwisho ya Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa 8 May 1945, mjini Algiers kocha wa Difaa El Jadidi alifanya kosa la kumuacha Msuva nje na kumuingiza kipindi cha pili, wakiwa nyuma kwa bao 1-0.

Kuingia kwa Anthony Okpotu na Msuva katika kipindi cha pili kuliiongezea nguvu Difaa ambayo hata hivyo iliponzwa na bao la dakika ya mwisho ya mchezo na kujikuta ikifungwa mabao 2-1.

Kutokana na kupoteza mchezo huo, Difaa imejikuta ikiporomoka hadi mkiani mwa Kundi B, ikiwa na pointi moja, baada ya timu zote kumaliza mzunguko wa kwanza, TP Mazembe ikiendelea kukaa kileleni, MC Alger wamepanda hadi nafasi ya pili na ES Setif inashika nafasi ya tatu.

Difaa itaikaribisha ES Setif kwenye uwanja wake wa El Abdi, mjini  El Jadida Julai 27 mwaka huu katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa lala salama.

Chanzo: mwananchi.co.tz