Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msudani wa Simba kuwatesa Ligi Kuu

68731 Pic+msudani

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO mpya wa Simba, Msudani Sharaf Eldin Shiboub, anatajwa kuwa tishio katika Ligi Kuu Bara ya msimu ujao, ikidaiwa ni mahiri wa pasi za mwisho, kuchezesha mpira na kasi.

Miraji Athuman naye ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Simba, iliomsajili kutoka Lipuli, hakusita kutoa hisia zake kwa Msudani huyo kwamba ni namba inayokuja kutikisa kwenye ligi.

Miraji amesema, Shiboub anajituma bila kuonyesha kutegea mazoezini, fundi wa pasi za mwisho, anamiliki vyema eneo la kati, akisisitiza kwamba ana vitu vingi.

Anaendelea kufunguka kwamba wachezaji wanajuana ubora wake na kwamba Msudani huyo anaamini atakuwa na jipya kama mchezaji wa kigeni kwenye ligi.

"Tusubiri ligi ianze ila nilivyomuona mazoezini kiukweli jamaa anajua kilichomleta bongo, mpambanaji kiasi kwamba utadhani hahitaji maelekezo mengi.

" Kiukweli anafanya hata wachezaji wengi kuiga mfano wake,  hii nzuri kwenye timu inasaidia kuwa na ushindani wa hali ya juu ya namba kisha kwenda kushindana dhidi ya wapinzani wetu,"anasema.

Mbali na kumzungumzia Msudani ameitazama nafasi yake ya kucheza ndani ya kikosi hicho kisha akatamka kwa ujasiri kwamba ana nafasi na anapenda kupambana hivyo anaamini atakuwa na msimu mzuri.

"Mpaka wananisajili waliona kitu kwangu, sitaki kuwaangusha, nitapambana mpaka nahakikisha napata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Patrick Aussems," anasema.

Chanzo: mwananchi.co.tz