Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshambuliaji wa Taifa Stars ageuka kinyozi Misri

63972 Pic+adi

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Taifa Stars, Adi Yussuf amekuwa kivutio kwenye kambi ya timu ya taifa 'Taifa Stars' inayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) huko Misri baada ya kujipa kazi ya kuwanyoa nywele wenzake.

Yussuf anayechezea Blackpool inayoshiriki Ligi Daraja la Pili England, ametumia ukurasa wake wa Twitter kuonyesha ufundi wake kama kinyozi.

Katika picha hizo, Yussuf ameonekana akiwanyoa washambuliaji wenzake wawili wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Picha hiyo imeonekana kuzua mijadala kwa mashabiki ambao wameitolea maoni tofauti ingawa mengi yamekuwa ni ya kumhamasisha mshambuliaji huyo na wenzake kuifunga Senegal katika mchezo utakaozikutanisha leo saa 2.00 usiku.

AFCON ni mashindano ya kwanza kwa Yussuf kuitumikia Taifa Stars baada ya benchi la ufundi chini ya kocha Emmanuel Amunike kuridhishwa na uwezo wake.

Awali Yussuf aliwahi kuitwa kikosini wakati Stars ilipokuwa chini ya Kocha Boniface Mkwasa lakini alikwamishwa na taratibu za uhamiaji.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz