Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshahara mmoja tu, Miquissone analipa Yanga yote

Luis Miquissone?fit=1200%2C800&ssl=1 Mshahara mmoja tu, Miquissone analipa Yanga yote

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MAPUTO. MKAZI wa hapa Maputo, Luis Jose amekula maisha nchini Misri. Staa huyo mkubwa kwenye soka la Bongo ambaye ameonekana jijini hapa juzi, ameuzwa na Simba kwa Al Ahly ya Misri.

Habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo jijini hapa ni kwamba atalipwa mshahara wa Dola 34,000 sawa na Sh80 milioni rekodi ya kujivunia Simba.

Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba kama mastaa wote wa kikosi cha kwanza cha Yanga wanalipwa Sh7milioni kama Mukoko Tonombe ni kwamba Luis kwa mwezi anawalipa wote na anabakiwa na chenji. Mshahara huo ni kadirio la juu kwani uhalisia ni kwamba wachezaji wengi wanalipwa chini ya hapo.Habari zinasema kwamba Simba imemuuza mchezaji huyo kwa Dola 900,000 zaidi ya Sh2 bilioni ambayo ni thamani kubwa zaidi katika miaka ya karibuni.

Habari zinasema Luis mbali na mshahara huo atakuwa anapokea posho za kufa mtu pamoja na Sh23 milioni kama pesa ya manunuzi kila msimu.

Licha ya kuwa na mchango mkubwa timu ya Taifa ya Msumbiji, Luis alikuwa mchezaji tegemeo Simba katika ligi ya ndani na michuano ya kimataifa.

Kabla ya kusaini alikuwa akihusishwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini lakini inadaiwa kwamba alikataa na kuchagua Ahly ambako kuna mkwanja mrefu.

IMEANDIKWA NA MOSES ADELINO

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz