Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Makata Alliance FC afunguka

24717 Pic+alliance TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Baada ya kuanza kwa sare ya bao 1-1, kocha mpya wa Alliance FC, Dady Gilbert amesema ana kazi nzito ya kuwafunda washambuliaji wake kufunga mabao.

Timu hiyo juzi ililazimishana sare ya bao 1-1 na Coastal Union, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha huyo mpya aliyebeba mikoba ya Mbwana Makata aliyejiweka kando baada ya kuibua mzozo na uongozi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Gilbert alisema ameona upungufu katika kikosi chake, lakini tatizo lipo kwa washambuliaji kutofunga mabao.

Kocha huyo amewataka wadau kumpa ushirikiano kuungana pamoja kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema katika Ligi Kuu na kukwepa janga la kushuka Daraja.

“Huu ni mchezo wangu wa kwanza, sitaki kuzungumzia matokeo, kiufundi nimeona makosa yalipo hasa safu ya ushambuliaji kwa hiyo nitatumia uwezo wangu kufanya maboresho ili kufikia malengo,” alisema Gilbert.

Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda alisema wapinzani wao walionyesha kiwango bora na ushindani na kuwatibulia mipango ya kupata pointi tatu.

Mgunda pia aliishauri Alliance kutulia kujipanga upya akisema timu hiyo yenye idadi kubwa ya wachezaji vijana itakuwa tishio msimu ujao.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz