Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpongo atoa darasa la usajili

MPONGO ED.webp Mpongo atoa darasa la usajili

Tue, 12 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA kipa wa Coastal Union ya Yanga, Juma Mpongo amewakata wachezaji wazawa kuwa makini katika suala zima la vipengele vilivyopo kwenye mikataba wanayoingia kipindi cha usajili.

Mpongo ambaye amewahi kuitumikia KCB ya Kenya inayoshiriki Ligi Kuu nchi humo, ameliambia Nipashe kuwa kuelekea kipindi cha usajili wachezaji hususan wazawa, wanapaswa kuwa makini kwa kusoma na kuelewa vema mikataba yao kipengele kwa kipengele kabla ya kusaini.

Alisema mara nyingi wachezaji wazawa wamekuwa wanasaini mikataba bila ya kusoma vipengele vya mikataba hiyo zaidi ya kuangalia kiasi cha fedha za usajili na mshahara.

"Sasa hivi soka la Tanzania liko vizuri na kibiashara kuliko wakati tumeanza sisi, hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa makini katika vipengele vya mikataba wanayoingia hasa kila kipengele kiwe kinabeba pande zote mbili.

"Ukiangalia katika mikataba wanayoingia wachezaji wazawa wanapoingia huwa kipengele cha endapo kuna timu kutoka nje itakapokuja basi klabu iwe rahisi kumruhusu, lakini pia wanatakiwa kuangalia zaidi maslahi yao katika mshahara kuliko ile ya kusaini," alisema Mpongo.

Alisema mikataba mingi ambayo wanaingia wachezaji wazawa waangalie vipengele vya kuwabeba siku wakiachwa au kupata timu nje ya nchi.

Mpongo alisema kutoka kwake nje ya nchi, amejifunza mambo mengi ikiwamo haki za mchezaji hasa kuingia mikataba na klabu husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live