Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpepo: Nilikatishwa tamaa kucheza soka

17747 Pic+mpepo TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mshambuliaji wa Singida United, Eliuter Mpepo ni mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho kutokana na uwezo wake wa kuwasumbua mabeki, kufunga na kutengeneza mabao. Amejiunga n timu hiyo akitokea Prisons ya Mbeya.

Mpepo alisema baada ya mkataba wake kumalizika, alitafuta timu itakayomtoa na Singida wamemwona.

Eliuter alishirikiana vyema na Mohammed Rashid kwenye eneo la mwisho la ushambuliaji la kikosi cha Prisons. Rashid kwa sasa yuko Simba.

Mikiki imepata nafasi ya kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo ambaye ameizungumzia safari yake ya soka huku akizitaja changamoto ambazo amekutana nazo.

Kabla ya kutua Prisons, Eliuter alizichezea Kinyerezi United ambayo ilikuwa madaraja la nne, Friends Rangers na Mbeya Kwanza za daraja la Kwanza.

Hata hivyo Eliuter anasema hawezi kusahau mazingira aliyapitia akiwa Friends Rangers kwa kusema ni kama yalimkomaza kisoka.

“Ulifika muda mpaka nikaanza kuwaza kuachana na soka, nilivyojiunga na Friends kuna baadhi ya viongozi walikuwa hawanipendi kabisa hivyo walinitengenezea majungu kwa hata kupandikiza chuki kwa mashabiki.

“Walifanikiwa kiukweli maana kila nilipokuwa naingia nilikuwa nazomewa, hali ya kuzomewa nilishindwa kuimudu mpaka ikaanza kuathiri uwezo wangu wa kawaida wa uwanjani nilipiga moyo konde lakini niliushinda ule mtihani,” anasema Eliuter.

Pamoja na kuonekana kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kwa sasa, Eliuter amesema hana tatizo wala mapenzi kati ya Simba na Yanga kama ukitokea upande wowote kumwitaji atakuwa tayari kuusikiliza.

“Namshukuru sana kocha wangu wa Tanzania Prisons, Mohammed Abdallah kwa kuniamini na kunipa nafasi na hata Singida United wakaniona na sasa nakula maisha huku,” anasema.

Chanzo: mwananchi.co.tz