Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpenzi aliyemchoma moto Rebeca Cheptegei ameaga dunia

Mpenzi Aliyemchoma Moto Rebeca Cheptegei Ameaga Dunia.png Mpenzi aliyemchoma moto Rebeca Cheptegei ameaga dunia

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha Rebecca Cheptegei Dickson Ndiema ameaga dunia katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret.

Hospitali hiyo ilithibitisha kuwa Ndiema alifariki Jumatatu usiku katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alikokuwa amelazwa.

Ndiema alifariki siku chache baaada ya Cheptegei kufariki katika hospitali hiyo hiyo ikidaiwa kuwa alimmwagia mafuta ya petroli kisha kumchoma moto, mbele ya watoto wake wawili.

Polisi walithibitisha kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa muda mrefu sana kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi ambacho Rebecca alikuwa akiishi.

Cheptegei atazikwa Jumamosi nchini Uganda. Atazikwa kwa heshima ya kijeshi.

Chanzo: Bbc