Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto umewaka Yanga, wachezaji watimka

87625 Pic+yanga Moto umewaka Yanga, wachezaji watimka

Thu, 12 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Yanga kumetibuka. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Sadney Urikhob kutimka klabuni hapo huku nyota wengine wakiandika barua za kuomba kuachana na klabu hiyo ya Jangwani.

Urikhob ambaye gazeti dada la Mwanaspoti liliwahi kuripoti kutoweka kwake kambini kwa siku kadhaa kabla ya kwenda Mwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu akishinikiza kulipwa fedha zake za mishahara, ameshatua kwao Namibia.

Hata hivyo, huku nyuma klabu yake imeandika barua ya kumuacha.

Akizungumza kutoka Namibia, straika huyo aliyetua msimu huu Jangwani alisema ametimkia kwao tangu juzi sababu ya kutomaliziwa fedha zake za usajili na kutolipwa mshahara wa miezi miwili mfululizo hivyo akaamua kuandika barua kuachana na klabu hiyo.

“Tangu baada ya mechi ya KMC niliamua kutimka zangu. Niliiandikia Yanga barua ya kuachana nayo kwa kushindwa kuheshimu makubaliano. Kusema kweli nilikuwa naishi kwa dhidi kwa kutolipwa fedha na viongozi hawakuwa wakweli, kila wanapoulizwa wanadai madai klabu haina fedha,” alisema.

Straika huyo ambaye ameondoka Yanga bila kufunga bao lolote kwenye Ligi Kuu, alisema sio yeye pekee aliyekuwa akiishi kwa dhiki tangu atue Yanga, lakini kwa kutambua kuwa ana kwao akaona isiwe shida ila kuamua kuomba kuachana na Yanga.

Alipoulizwa kama ikitokea akahitajiwa na timu za Tanzania, alisema ni ngumu kwake kurudi kwani kwa kipindi kifupi amebaini kuwa soka la Bongo linaendeshwa kibabaishaji mno licha ya kuwa na mashabiki wengi wanaopenda mchezo huo.

“Siwezi kurudi Tanzania, ila wewe fahamu kwa sasa mimi ni mchezaji huru na kokote naweza kujiunga kucheza, ila siwezi kuja huko, soka la kwenu linaendeshwa kijanja na ubabaishaji mwingi,” alisema Urikhob.

LAMINE MORO

Mbali na Urikhob aliyeamua kuomba kuachwa Jangwani, taarifa zaidi zinasema beki wa kati, Lamine Moro naye ni kati ya walioomba kuachwa na klabu hiyo kutokana na sababu kama za Mnamibia huyo.

Lamine Moro naye ameomba kuachwa na klabu hiyo, huku taarifa za ndani zinadai kuwa, Patrick Sibomana, Juma Balinya na David Molinga nao ni kati ya wanaotaka kutimka katika timu hiyo.

Awali Mwananchi ilipenyezewa taarifa kwamba hata baadhi ya wachezaji wa ndani nao wameanza kuonja joto ya jiwe ya maisha ya Jangwani, lakini wanausikilia uongozi uliowahidi kuwalipa malimbikizo ya mishahara yao.

Hata hivyo, uongozi wa Yanga, kupitia Katibu Mkuu wake, David Ruhago ulipoulizwa kuhusu tuhuma za wachezaji kudai fedha za usajili na mishahara ya miezi ya nyuma, walidai hilo ni suala lao binafsi na anashangaa kuona wachezaji wamekuwa wakilalamika kwa vyombo vya habari

Chanzo: mwananchi.co.tz