Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Monalisa amkinga Sonia na mafisi

Monalisa Pic Data Monalisa amkinga Sonia na mafisi

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KATIKA kuhakikisha mtoto wake anamlinda na mafataki kwenye tasnia ya muziki, msanii Monalisa huwa akiwaagiza kaka zake wampeleke na kumsubiria mtoto wake akiwa studio.

Mtoto huyo anayeitwa Sonia, ameingia katika tasnia ya muziki na tayari ametoa vibao mbalimbali ikiwemo ‘Mama Yake Sofia’ na ‘Bye’ alichokiachia wiki hii.

Katika mahojiano na Jiachie iliyotaka kujua ni namna gani anamlinda mwanaye na mafataki wa kwenye tasnia kutokana na watoto wa kike kupitia zaidi changamoto hizo, Monalisa alisema huwa akimpeleka mwenyewe studio na kumsubiria hadi anapomaliza na pia kazi hiyo wanaifanya wajomba zake.

“Nipo kwenye tasnia ya sanaa kwa muda mrefu sasa hivyo mambo yanayofanyika yote humo ikiwemo hawa mafataki nayajua, hivyo nina kila sababu ya kumlinda mtoto wangu na watu wa aina hii kwa kumsindikiza anapokuwa kwenye shughuli zake za kimuziki.

“Pia kama kuna wakati nimebanwa huwa nawaomba wajomba zake wamsimamie na kuhakikisha wanarudi naye nyumbani kwani licha ya sasa kufika umri wa kuitwa mtu mzima, bado kama mama nina jukumu la kumlinda aweze kufikia ndoto zake,” alisema Monalisa.

Akizungunmzia msanii anayemvutia bintiye hapa Bongo, alisema “Sonia humwambii kitu na Ruby”.

Sonia mwaka huu amehitimu kidato cha sita Shule ya Sekondari Tusiime alikochukua masomo ya biashara (ECA).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz