Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Molinga, Mustapha kuwakosa Waarabu

80773 Pic+molinga Molinga, Mustapha kuwakosa Waarabu

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WACHEZAJI wa Yanga, David Molinga na Mustapha Suleiman wameondolewa kwenye kikosi kinachotarajia kuivaa Pyramids FC mchezo unaotarajia kuchezwa Oktobar 27 mwaka huu. Wachezaji hao wataukosa mchezo huo kutokana na usajili wao kuchelewa hivyo majina yao yalishindwa kupitishwa kwa wakati. Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela alisema wachezaji hao watatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu na mechi ya kimataifa endapo watafuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. "Ni kwa mujibu wa kanuni, sisi tulitamani kuona wanajumuika katika mchezo huo lakini imeshindikana kutokana na kanuni zinavyoelezwa," "Kukosekana kwa wachezaji hao hakutunyimi ushindi kwenye mchezo ulio mbele yetu tunaimani na nyota waliopo tunaamini wanaweza kutupa matokeo mazuri," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz