Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mogella: Yanga hii mbona bado sana

82546 Pic+yanga Mogella: Yanga hii mbona bado sana

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogela amesema zaidi ya nusu ya wachezaji wa Yanga hawana sifa ya kuichezea timu hiyo kongwe ya soka nchini. Mogella amekwenda mbali zaidi na kusema kama timu hiyo itaweza haina budi kuachana nao kwani hawana msaada. "Zaidi ya nusu ya kikosi cha Yanga ni dhaifu, sio tu kimataifa hata kwenye ligi bado ni tia maji tia maji," alisema nyota huyo wa zamani. Alidai kwa ukubwa wa Yanga na aina ya wachezaji waliopo haiendani. "Ingetumia kipindi cha dirisha dogo kuongeza nguvu, lakini kwa timu ninayoiona Yanga, hata kwenye ligi watapata tabu. Huku akitolea mfano kwenye safu ya ushambuliaji, Mogella alisema timu hiyo ilihitaji kusajili wachezaji wa kiwango cha Heriter Makambo ambaye aliuzwa kwenye usajili uliopita. "Sijui kama uongozi unakubaliana na aina ya wachezaji waliopo, si wa kuamua matokeo, kama timu isipobadilishwa watahangaika mno si kimataifa tu hata kwenye ligi," anasema Mogella. Anasema zaidi ya nusu ya wachezaji waliopo Yanga hawana sifa za kuitumikia timu hiyo kutokana na viwango vyao na ukubwa wa klabu wanayoichezea. "Yanga inapaswa kubadilika na kuweka vipengere vya masharti kwenye mikataba ya wachezaji wao ili viweze kuwabana na wasipofikia malengo waachane nao.

Chanzo: mwananchi.co.tz