Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo alivyombadilikia Chama kisa Manara

Chamaaama Data Clatous Chama

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STAA wa Simba, Clatous Chama jana jioni ameonja joto ya jiwe baada ya kuchenjiwa kibao na muwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kisa Haji Manara.

Chama akiwa Live Insta kwenye mkutano wake na mashabiki ambao Mo alikuwemo, aliulizwa swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya klabu ya Simba, kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilionekana kumchefua Mo.

Mo alimuuliza Chama "Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho?" Chama akiwa anamjibu Mo alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo akamuuliza tena Nani aliyekulipa Ada....Haji?  baadae Chama alipotaka kujibu Mo akamwambia anatoka kwenye mkutano huo.

Awali kwenye majadiliano na mashabiki, Chama alimuomba Mo kuendelea kubaki Simba kwa kumuahidi kufanya vizuri ili aweze kupata faida.

Chama alisema kiongozi yeyote anayeipa mafanikio anapitia changamoto hivyo hata kwa upande wake anatakiwa kulibeba lililotokea kama changamoto na sio kujiondoa kwenye taasisi ambayo inategemewa na wengi.

"Simba sio ya mtu mmoja kukosea kwa mmoja kusiwaharibie kazi wengine ambao wanaendesha familia zao kupitia timu hiyo, kuna Mohammed Husein 'Tshabalala', mimi mwenyewe, Shomari Kapombe ukiondoka unawanyima haki," alisema.

"Ili kuweza kukuingizia faida kama wachezaji tunakuahidi kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na kimataifa ili tuweze kutwaa mataji ambayo yatakuongezea manufaa kwa njia moja au nyingine," alisema.

Pia, alimuomba Mo kuachana na yaliyopita aangalie namna ataiweka timu kwenye mazingira mazuri ya kutetea taji ikiwa ni sambamba na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aidha alimpongeza Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez kwa kufikia malengo waliyokuwa wamejipangia mwanzoni mwa msimu kutwaa taji la ligi, kombe la Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) na kufika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa.

"Pia naomba nikupongeze kwa hatua uliyoichukua kufuatia kinachoendelea baina yake na Haji Manara”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz