Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Ibrahim, Ndemla wapewa mchongo wa maana

60894 Pic+mo

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

IBRAHIM Mohamed 'Mo Ibrahim' na Said Ndemla wa Simba wamepewa mchongo wa namna ya kuhakikisha wanapiga pesa ndefu kutokana na vipaji vyao.

Jambo la kwanza waliloshauriwa na wadau wa soka nchini ni kuamua kujituma katika mazoezi  yao binafsi yatakayowaweka fiti kisha wapambanie nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.

Emmanuel Gabriel ni staa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, amewataka wachezaji hao kuamua kubadili mfumo wa namna ya kufanya kazi zao.

"Hakuna kocha ambaye anaweza kumwacha mchezaji ambaye ana uwezo wa kuibeba timu, Mo Ibrahim na Ndemla wakicheza msimu mmoja kwenye kikosi cha kwanza basi itakuwa habari nyingine.

" Kwa timu za hapa Tanzania sijaona ambayo anaweza akaichezea Ndemla kwa kiwango chake labda aende Yanga ama Azam FC lasivyo anastahili kucheza nje.

"Tatizo pia lipo kwa watu ambao wanawasimamia wanakubali vipi wateja wao wanakuwa hawana namba, nadhani wachezaji wenyewe wajitathimini" anasema.

Naye Zamoyoni Mogella anasema wachezaji hao hawajajitambua kwamba wamekalia mamilioni ya pesa kwa kubabaika na viposho ambavyo wanavipata.

"Wakiamua kufanya kazi wana mamilioni ya pesa kuliko ambazo wanapata kwa sasa, waige mfano wa Mbwana Samatta na Simon Msuva hao sasa wanazungumzwa kwenye Bilioni na sio Milioni walijielewa mapema, hivyo wawe na wivu wa maendeleo, wapo wengi sio Ndemla peke yake" anasema.

Chanzo: mwananchi.co.tz