Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Banka apania makubwa Yanga

14078 Pic+banka TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa ‘Banka’ amejawa na shauku ya kuanza kuitumikia Yanga kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi kutwaa ubingwa.

Banka ambaye amejiunga na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili anauwezo wa kucheza kama kiungo wa kati (8) pia nyuma ya mshambuliaji (10) na hata winga ya kulia au kushoto.

Issa mwenye asili ya Zanzibar amezungumza na Spoti Mikiki na kuelezea mambo kadhaa ambayo wadau wengi wa soka hawafahamu kuhusu yeye hasa alipoanzia kucheza soka.

“Kuna timu moja ya mtaani inaitwa Jamaica ya Zanzibar hiyo ndiyo nilianza kuichezea wakati nikiwa mdogo, 2010 hadi 2013 ambapo nilianza sasa kuangaikia kwa kutafuta timu kubwa ya kuichezea,” anasema Issa.

Changamoto

“Nimepitia mengi sana lakini kikubwa ni changamoto ya kutokuwa na jina kubwa, ilinifanya kuwa na wakati mgumu sana, hakuna aliyekuwa anajali kuhusu mimi mpaka pale atakaponiona nacheza. “Mtibwa nilifanya majaribio na kufuzu ila ilibidi kuanza kuonyesha kwa nguvu zote ili nianze kujijengea jina, kwa kiasi chake nimefanikiwa, ukiwa haufahamiki ningumu sana kwenda sehemu na kupata nafasi moja kwa moja,” anasema.

Mavazi

“Sio mtu wa mambo mengi kwenye mawazi, mara kwa mara navaa tisheti na jinzi ila sio kwamba ndiyo nguo ninazo zipenda, huwa napenda sana kuvaa suti ila tatizo lile ni vazi ambalo huwezi kulivaa kila wakati,” anasema Issa.

Msosi

“Mmmmh!! Huniambii kitu kwenye wali na Samaki, hakuna chakula ninachokipenda zaidi ya hicho” anasema kiungo huyo aliyezaliwa Desemba 17, 1995.

Malengo

“Wachezaji wengi wa hapa nyumbani maisha yao ya mpira huishia Yanga na Simba, sipendi na kwangu iwe hivyo natamani sana kama nitashindwa kufika Ulaya basi nicheze hata Ligi ya Afrika Kusini,” anasema Issa.

Chanzo: mwananchi.co.tz