Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnata, Makame kuifuata Yanga wiki ijayo

80770 Pic+metacha Mnata, Makame kuifuata Yanga wiki ijayo

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIPA  Metacha Mnata na kiungo Abdulazizi Makame wa Yanga, Jumatatu wataungana na nyota 24 watakaotangulia jijini Mwanza tayari kwaajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara na mechi ya awali ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri. Nyota hao wawili wapo kwenye majukumu ya timu ya Taifa 'Taifa Stars' inayoshuka dimbani usiku wa leo Ijumaa kumenyana na Sudan mchezo wa kufuzu fainali za Chan. Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kesho Jumamosi nyota 24 wanatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam alfajiri kuelekea Mwanza tayari kwa mechi hizo mbili. "Yanga tuna michezo miwili muhimu Kanda ya Ziwa mmoja ni mchezo wa ligi dhidi ya Mbao Oktoba 22 na mchezo wa Kombe la Shirikisho Oktoba 27 mwaka huu," alisema. "Maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri wachezaji wote wapo fiti isipokuwa Issa Bigirimana na Mohamed Issa 'Banka' ambao bado wapo chini ya uangalizi wa daktari," alisema Mwakalebela.

Chanzo: mwananchi.co.tz