Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwara tu! Mazembe yatua Mbeya kwanza kabla ya kuifuata Simba Dar es Salaam

50343 PIC+MAZEMBE

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Taarifa zinasema kikosi cha TP Mazembe kitatua Dar es Salaam kikitokea Mbeya ambako walitua kwa muda, huku wakihofia kupanda basi waliloandaliwa na wapinzani wao Simba kwa hofu ya hujuma.

TP Mazembe inatarajiwa kutua Dar es Salaam majira ya saa 10:30 tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo finali.

Mtu wa karibu wa TP Mazembe anayejulikana kwa jina moja la Patrick amesema, ndege hiyo itaweka kituo Mbeya wataweka mafuta na mambo mengine.

Amesema, ndege hiyo ambayo imebeba wachezaji,  benchi la ufundi na viongozi, safari yake ilianzia Afrika Kusini ambako ndiko hukaa. Ilikwenda Lubumbashi kwa ajili ya kubeba wachezaji wao na kituo kingine ni Mbeya kabla ya kufika Dar es Salaam.

Jamaa huyo ambaye ndiye alikishughulikia ujio wa TP Mazembe ilipokuja kucheza na Yanga 2016, mashindano kama haya.

"Msafara utatua muda ya saa kumi. Ni ndege binafsi lakini kabla ya Dar es Salaam itatua Mbeya kwa ajili ya sevisi," alisema.

Amedokeza, upo uwezekano wa TP Mazembe kutotumia basi ambayo wameandaliwa na wenyeji wao Simba.

Amesema, inafanyika mipango ya kuleta basi nyingine itakayobeba wachezaji wao wakihofu hujuma.

HALI YA UWANJA WA NDEGE

Kumekuwa na hali ya sintofahamu kuwa ndege hiyo itatua uwanja wa ndege wa zamani (terminal 1) au wa sasa (terminal 2) kwani hata wahusika wanatoa taarifa zinazokinzana.

Wapo wanaosema ni binafsi itatua wa zamani na wengine kwa sababu ni ya kimataifa hata kama ni binafsi itatua wa sasa.

Hata hivyo basi pamoja na magari ya mapokezi yaliyoandaliwa na watu wa Simba yapo uwanja wa sasa.

Lakini, kupitia jamaa huyo wa Congo amesisititiza TP Mazembe watatua kupitia uwanja wa sasa (terminal 2)

Hali ya uwanjani hapa ni tulivu na wanaonekana makumi ya mashabiki wa TP Mazembe ambao wamefika kwa ajili ya kupokea timu hiyo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz