Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude amfuata okwi kwa pipa Zenji

34539 Pic+mkude Tanzania Web Photo

Wed, 2 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba kimeondoka leo Jumatano kuelekea Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi na Ijumaa watacheza mechi ya kwanza.

Simba waliondoka saa 3;30 asubuhi na boti aina ya Kilimanjaro 4, huku wakiwa na kumbukumbu ya kuondolewa katika hatua ya makundi msimu uliopita kikosi hiko kikiwa chni ya kocha Mrundi Msoud Djuma.

Mpaka Mwanaspoti inaondoka Bandari ambapo kikosi cha Simba kiliondoka saa 3:30 asubuhi wachezaji wanne wa Simba hawakuonekana katika msafara huo ambao mchana ulitua Visiwani Zanzabar.

Wachezaji hao ni nahodha John Bocco, Emmanuel Okwi, Jonas Mkude na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Daktari wa Simba Yassin Gembe alisema Okwi siku zote huwa awezi kusafiri kwa boti kwa maana hiyo amepanda ndege na ataanza kufika kabla yao na kisha mchana wataungana kwa pamoja.

“Kuhusu Mkude na Bocco nao huenda watakuwa wamepanda ndege kama Okwi lakini Dida sijafahamu ila nadhani nikishafika Zanzibar tukiwa kwa pamoja nitakuwa na majibu sahihi lakini tumeondoka na wachezaji wote na wala hakuna hata majeruhi hata mmoja,” alisema Gembe.



Chanzo: mwananchi.co.tz