Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude Avuruga Tena Simba

Mkude2.png Mkude Avuruga Tena Simba

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

IMEFICHUKA kuwa, sababu kubwa ya kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude kushindwa kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, ni kitendo cha mchezaji huyo kukosa ripoti ya vipimo vya afya.

Wachezaji 24 wa Simba waliondoka jioni ya Ijumaa kwa ndege ya kukodi kuelekea Gaborone, Botswana kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana na Simba kushinda 2-0.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba kimelitonya Spoti Xtra kuwa, Mkude alishindwa kusafiri kutokana na kukosa ripoti ya vipimo vyake vya afya ambavyo ni miongoni mwa mahitaji ya lazima kwa wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo mikubwa Afrika.







“Ishu nzima ilikuwa hivi, siku chache kabla ya safari ya kuelekea Botswana kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Galaxy, wachezaji na viongozi wote tulienda kufanya vipimo kwenye moja ya hospitali kubwa hapa nchini iliyopo Dar es Salaam (jina tunalo), akiwemo Mkude lakini baada ya kufika hospitalini hapo, Mkude akatoweka katika mazingira ya kutatanisha, licha ya juhudi za kumtafuta lakini hakupatikana.

“Cha ajabu siku ya pili alikuja kwenye mazoezi kama kawaida na alipoulizwa kuhusiana na kilichotokea hospitalini akajibu angekwenda kupima lakini haikuwa hivyo mpaka siku tunaondoka, alipoleta pasi yake ya kusafiria akaambiwa hawezi kusafiri kwa kuwa hana ripoti ya afya,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa Simba, Murtaza hakitakuwa na mabadiliko, badala yake ataendelea kuwatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza akiwemo Diarra, Fiston Mayele, Shaban Djuma, Jesus Moloko na Yannick Bangala.

“Kocha amepanga kuchukua pointi tatu katika kila mchezo, hiyo ni kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu ya ubingwa tuliyojiwekea.“Tayari tumechukua pointi sita katika michezo miwili mfululizo ya ligi tuliyocheza dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold, pia anazitaka na hizi za KMC.

“Jana usiku kocha alifanya kikao na wachezaji wake wote mara baada ya chakula cha jioni sambamba na kuangalia video za mechi mbili za mwisho za ligi ambazo KMC imecheza kwa lengo la kuangalia upungufu na ubora uliokuwepo kwao,” alisema Saleh.Akizungumzia mchezo huo, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, alisema wamejiandaa vema na kikubwa wanahitaji pointi tatu.

“Hatuangalii tunacheza na nani, kikubwa benchi letu la ufundi limefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha tunapata ushindi ambacho ndiyo kitu cha umuhimu ketu,” alisema Mwagala.Rekodi zinaonesha kwamba, timu hizo zimekutana mara sita kwenye Ligi Kuu Bara ambapo Yanga imeshinda tatu, KMC imeshinda moja na sare mbili.


“Nianze kwa kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya na kujitahidi kufuata maelekezo ambayo nimekuwa nikiwapa mazoezini ambayo mwisho wa mchezo tukafanikiwa kupata ushindi.

“Wachezaji wangu wamefanya kitu kikubwa, kwani unapocheza ugenini siyo lazima kucheza soka la kuvutia badala yake unatakiwa kucheza kwa nidhamu ya kujilinda.“Wakati ukijilinda unatakiwa kutumia vema kila nafasi unayopata kama wachezaji wangu walichofanya leo (juzi), nawapongeza sana kwa hilo.

“Bado hatujamaliza kazi, bado tuna kibarua kigumu nyumbani tutakapocheza mchezo wa marudiano, Galaxy siyo timu nyepesi, hivyo hatutaki kupoteza nyumbani,” alisema Gomes.


Mangungu kuzungumzia hilo, ambapo alisema: “Suala la Mkude kutosafiri na timu ni benchi la ufundi ndilo linaweza kutoa maelezo mazuri.“Hii ni kwa sababu wao ndiyo wanajua wachezaji gani wanawahitaji kuendana na wapinzani wetu, hivyo nadhani ni maamuzi ya benchi la ufundi kuendana na uhitaji wa mchezo.

”Hii si mara ya kwanza kwa Mkude kuripotiwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika kikosi hicho ambapo mwishoni mwa msimu uliopita, Simba walilazimika kumuondoa katika kwenye mipango yao kutokana na vitendo hivyo kabla ya kurudishwa tena kikosini msimu huu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz