Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude, Ajibu waachwa AFCON

61638 Pic+astars

Fri, 7 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA  wa Simba na Yanga, Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu wameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kinachoelekea  Misri kujiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika  'AFCON'.

Kikosi cha wachezaji 32 kinatarajiwa kuondoka leo Ijumaa kwa ajili ya kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Misri ambako fainali hizo zitafanyika.

Ajibu na Mkude hawakuwa sehemu ya kikosi hicho, kilichofanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mbali na nyota hao wachezaji wengine walioachwa ni Shomary Kapombe wa Simba aliyetoka majeruhi, Kennedy Wilson wa Singida United, Kassim Hamis wa Kagera Sugar na Ally Ally wa KMC.

Kinda wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17  'Serengeti Boys', Kelvin John 'Mbappe' ni miongoni mwa mastaa 32  watakaosafiri kuelekea Misri.

Mara baada ya kikosi cha Stars kutua Misri wataungana na Himid Mao ambaye alikuwa akimalizia majukumu ya kuinusuru Petrojet nchini humo isishuke daraja.

Kwa mujibu wa benchi la ufundi la  Stars, likiongozwa na kocha Emmanuel Amunike, wakiwa Misri kutafanyika tathimini itakayowasaidia kubaki na wachezaji 23 watakaotumika kwenye fainali hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz