Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkongwe Kavila ataka pointi tatu za Mwadui

35088 Pic+mkngwe Kavila

Mon, 7 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila amesema wamejindaa leo kuvuna pointi tatu mbele ya Mwadui FC mkoani Shinyanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania, utakaochezwa, uwanja wa Mwadui Complex.

Kagera Sugar ambao wamecheza michezo 18, wapo nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 25 huku wenyeji wao, Mwadui ambao wamecheza mara 19, wamejikusanyia pointi 21 katika nafasi ya 12.

Kavila alisema kikosi chao kwasasa kipo kwenye hali nzuri tofauti na kipindi fulani ambapo walipoteana kwa kufanya vibaya kwenye michezo mfululizo ya Ligi.

“Tumejiandaa na naamini tunaweza kupata matokeo ya ushindi hata kama tupo ugenini, Mwadui ni wazuri kwa hiyo ni mategemeo yetu mchezo kuwa wa ushindani.

“Hatutarajii kuondoka mikono mitupu Shinyanga, alama tatu zitatuweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza kwenye nafasi za juu, mzunguko wa pili miaka yote unakuwaga mgumu lakini tatapambana mpaka kieleweke,” alisema Kavila.

Kiungo huyo mkabaji, alisema idadi kuwa ya wachezaji wenye uzoefu kwenye kikosi chao ilisaidia kwa kiasi kukubwa kurejea kwenye kiwango chao cha kawaida.

Kavila ambaye bado ananguvu na uwezo wa kuendelea kupambana na vijana, anakaribia miaka 40, alianza kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye miaka ya 90, akiwa na Coastal Union ya Tanga.



Chanzo: mwananchi.co.tz