Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa Lwandamina Wamalizika Azam, Apewa Shavu

George Lwandamina Joins Azam Mkataba wa Lwandamina Wamalizika Azam, Apewa Shavu

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

LICHA ya kuwa na matokeo mabaya msimu huu Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja wa kuzidi kukinoa kikosi hicho. Lwandamina alijiunga na Azam msimu uliopita baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu Mromania, Aristica Cioaba.

Mpaka sasa Azam imecheza mechi nne za ligi huku akishinda moja dhidi ya Namungo kwa bao 1-0, wakatoka sare na Coastal Union ya 1-1, wakafugwa mabao 2-1 na Polisi Tanzania na Yanga juzi wakawachapa mabao 2-0.

Azam pia imetolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufugwa bao 1-0 na Pyramid kwenye mchezo wa marudiano baada ya suluhu Uwanja wa Chamazi.

Akizungumza na Global Publishers, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria ‘Zakazakazi’amesema kuwa, pamoja na kocha huyo kumaliza mkataba bado wana mpango naye.

“Kiukweli sina taarifa kama kocha anataka kufukuzwa ndiyo maana hizo ni tetesi ila hakuna hata mpango wakuondolewa.

“Mkataba wake umeisha leo (jana) na kesho (leo), atasaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia Azam,” alisema ofisa habari huyo.

HII sasa sifa! ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kauli ya kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye ameweka wazi kuwa ubora wa sasa wa Yanga ni asilimia 45 tu ya kile anachokitaka, na baada ya muda watakuwa na timu ya kutisha zaidi.

Yanga juzi Jumamosi wakiwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, waliendelea kasi yao ya ushindi baada ya kuichapa Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Bara.

Kutokana na ushindi huo Yanga imezidi kujiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi zao 12, katika michezo minne waliyocheza.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Nabi alisema: “Kwanza nawapongeza sana wachezaji wangu kwa kuonyesha uwezo mzuri kwenye mchezo dhidi ya Azam, tumepata ushindi dhidi ya timu bora lakini licha ya ushindi huo na ubora tulionao naweza kusema kwa sasa timu yetu inacheza kwa asilimia 45 au 50 pekee ya kile nachohitaji.

“Mwanzoni mwa msimu huu niliomba miezi mitatu kutengeneza kikosi, na nikuhakikishie kuwa kwa mwenendo tuliaonao baada ya mwezi mmoja tutakuwa na kikosi kitakachotisha zaidi.

“Malengo yetu makubwa ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu na kwa usajili wa wachezaji na benchi bora la ufundi ambao umefanyika kwa udhamini wa GSM naamini tutafanikisha lengo hilo.”

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Chanzo: globalpublishers.co.tz